CHANJO YA CORONA NI SALAMA:RC MAKALLA






- Asema yeye na wote Waliochanjwa Jana wapo Salama.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla ametoa wito kwa Wananchi kuhakikisha wanapokea Chanjo ya Corona kwa *mustakabali wa Afya zao.*


*RC Makalla* ametoa kauli hiyo akiwa ni *miongoni mwa Viongozi waliopokea Chanjo hiyo wakati wa uzinduzi uliofanyika siku ya Jana* ambapo amesema *tangu amepokea Chanjo hiyo hajapata madhara yoyote ya kiafya.*


Aidha *RC Makalla* amempongeza *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha mfano* kwa kuchanja na *kutimiza wajibu* wake wa kuwaletea wananchi Chanjo ili Waweze *kuchanja kwa hiyari.*


Pamoja na hayo *RC Makalla* ameendelea kuwasisitiza *Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Corona* huku akisisitiza *uvaaji wa Barakoa wawapo kwenye Vyombo vya usafiri na suala la Level seat.*


Hayo yote yamejiri wakati wa ufunguzi wa *Kikao Cha tathimini ya Lishe Mkoa wa Dar es salaam* kilichohudhuriwa pia na *Waziri wa Afya Mhe. Doroth Gwajima.*


Akizungumza Katika kikao hicho *RC Makalla* amezielekeza *Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha zinatenga fedha za kuwawezesha Maafisa Lishe kutekeleza majukumu yao.*


Hata hivyo *RC Makalla* amewataka *Maafisa Lishe kuhakikisha wanatoa Elimu ya kutosha kwa Wananchi* kuhusu suala zima la *Lishe* ili kuepuka magonjwa mbalimbali ikiwemo *Udumavu na utapiamlo.*


*Itakumbukwa kuwa Wakuu wa Mikoa yote nchini walisaini mikataba ya uboreshaji wa Lishe Katika maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha jamii inakuwa na Afya Bora na Lishe Bora.*

0/Post a Comment/Comments