Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde ametoa rai kwa shule zote za bweni nchini kuweka vizima moto (fire extinguisher) na vitambuzi vya moto (smoke detector) ili kukabiliana na ajali za moto unapoanza katika mabweni ili kuokoa uhai wa wanafunzi na mali zao mala baada ya kuzuka kwa wimbi la kuungua kwa shule bweni.
Ametoa rai hiyo mala baada ya kutembelea shule ya sekondari Geita ambayo iliunguzwa moto mala tatu na baadhi ya wanafunzi ndani ya siku saba na kutaka elimu ya kujikinga na majanga ya moto itolewe na jeshi la zimamoto na uokoaji nchini ili kunusulu mali nyingi za shule na uhai wa wanafunzi.
Aidha Naibu waziri Silinde ametaka wanafunzi wote watakao bainika bila kuonewa kuwa wameshiriki katika kuunguza mali za shule hiyo hatua kali za kinidhamu zichukuliwe juu yao na mali za shule wazazi wao watahusika katika kuzirudishia kwa gharama zao ili iwefundisho kwa wanafunzi wengine weje tabia mbaya na kutaka walimu wa shule hiyo kukazania nidhamu shuleni hapo baada ya kuonekana nidhamu ya wanafunzi kua chini.
Ameongeza kua kwasasa vipindi vya dini viwe vya lazima kufundishwa katika shule zote licha ya kutokufanyoa mtihani kwani inaonekana wanafunzi ambao wanahofu ya mungu hawawezi fanya utovu wa nidhamu kuchoma mali za shule na vitendo vingi vya moto vinaonesha watoto wengi hawana hofu ya mungu ukitofautisha na shule ambazo wanakazania vipindi vya dini.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Geita Isaya Busagwe amesema shule yao ilikumbwa na ajali ya moto tarehe 5,6 na 14 mwezi huu wa saba katika miundombinu ya madarasa ya kidato cha sita na bweni lenye wanafunzi themanini viliathiriwa vibaya na moto na mpaka sasa umebainika baadhi ya wanafunzi wa kutwa kuhusika na matukio hayo kuchoma moto.








Post a Comment