Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Tanzania Dkt Noel Lwoga wa tatu kutoka kushoto na Mkurugenzi Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale, Zanzibar Bw Salim Sururu wa nne kutoka kushoto wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hizo baada kikao cha kuboresha mashirikiano kati ya taasisi hizi mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa yupo kwenye ziara kisiwani Zanzibar kwa ajili ya kujadili maeneo mbalimbali ambayo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana katika uhifadhi na uendelezaji wa Urithi wa Kale nchini Tanzania.
Kikao hicho kimeadhimia kuwepo na Mashirikiano kwenye masuala ya utafiti, ukarabati wa majengo ya kale, uhifadhi, uendelezaji wa malikale na utalii wa kihistoria ikiwemo matamasha na makongamano.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga
amekutana pia na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar (STCDA) Bi
Madina Haji Khamis (katikati) ili kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa Miji
Mikongwe ya Kale, na hasa kuadhimia kushirikiana katika usikamizi na ukarabati
wa Majengo ya kale, ikiwamo yale ya Mji Mkongwe wa Mikindani.


Post a Comment