Na Richard Mrusha
Naibu waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja amewasili katika Hifadhi ya Ngorongoro kwa ziara kikazi ya siku 3 ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kugawa mizinga ya nyuki 1500 kwa vikundi vya ufugaji nyuki vilivyoko ndani na pembezoni mwa hifadhi kutoka Wilaya za Karatu na Monduli Mkoani Arusha.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo tarehe 13 agosti, 2021 Mhe naibu waziri amekutana na Menejimenti ya NCAA na kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo.
Siku ya Jumamosi Mhe. Masanja atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa zoezi la kugawa Mizinga ya Nyuki kwa vikundi vya ufugaji Nyuki ndani na nje ya Hifadhi kwa lengo la kudhibiti wanyamapori waharibifu, pia atakagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Seneto hadi Kreta na kutembelea Ngorongoro kreta kukagua ikolojia na athari za mimea vamizi.
Aidha tarehe 15 agosti, 2021 Mhe Naibu Waziri atatembelea eneo la Ndutu linalopendekezwa kujenga mradi wa Faru na mwisho atatembelea maeneo mbalimbali ya Hifadhi kuangalia changamoto ya ma bykazi na shughuli za kibinadamu.
Mwisho.

Post a Comment