Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amemtaka Mkandarasi wa *kampuni ya JASCO* anaetekeleza Mradi wa Ujenzi wa *Barabara ya Makongo* kuhakikisha Mradi huo unakamikika na kukabidhiwa kabla ya *October 08 mwaka huu* baada ya *kutoridhishwa na utendajikazi wa Mkandarasi huyo.*
*RC Makalla* ametoa maelekezo hayo wakati wa *ziara ya ukaguzi* kwenye Barabara hiyo ambapo ameonyesha *kuchukizwa na tabia ya mkandarasi* huyo *kuonekana eneo la kazi siku pekee ambayo Viongozi wanatembelea* Barabara Jambo linalosababisha *kusuasua kwa Mradi* huo kuleta *kero na mateso* kwa Wananchi.
Aidha *RC Makalla* amesema tayari *DAWASA, TANESCO na TTCL* wameondosha miundombinu yao na wananchi wote wamelipwa *fidia* walizokuwa wakidai hivyo *haoni sababu yoyote ya mkandarasi huyo kuchelewesha Mradi.*
Hata hivyo *RC Makalla* amewaelekeza *TANROAD* kuhakikisha wanamsimamia ipasavyo mkandarasi huyo ili *Ujenzi wa Barabara ukamilike kwa wakati.*
*Barabara ya Makongo Ina urefu wa Km 4.5 na ujenzi wake unagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 8 ambapo ikikamilika inatarajiwa kurahisisha usafiri kwa Wakazi wa Makongo na kupunguza msongamano wa magari kwenye Barabara ya Bagamoyo.*

Post a Comment