Kutokana na kukwama kwa shughuli za uokoaji zilizozuiliwa na mvua kubwa vifo vinatarajiwa kuongezea kwenye Visiwa vya HAITI baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 7.2 kuikumba visiwa hivyo Jumamosi iliyopita.
Mamlaka za uokoaji nchini humo zimesema hospitali zimepungukiwa vifaa na kuelemewa idadi ya wagonjwa, mpaka sasa zaidi ya watu 1,941 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na tetemeko hilo huku majeruhi wakiwa zaidi ya 10,000 na watu wengine hawajulikani walipo.
Haiti imekumbwa na mfululizo wa majanga ya asili katika miaka iliyopita, pamoja na Kimbunga Matthew mnamo 2016.
Tetemeko la ardhi linalokumbukwa lililosababisha athari zaidi ni la mwaka 2010 ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 200,000 na kuzua hitilafu uharibifu mkubwa kwa miundombinu na uchumi wa nchi hiyo.
#TimesFMDigital


Post a Comment