WAFANYABIASHARA AFRIKA MASHARIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO.

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Profesa Kitila Mkumbo  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika  Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki  katika wiki ya viwanda mwaka 2021 ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa Julias Nyerere jijini Dar es salaam  

Rais wa Chama cha Biashara, Viwanda na Kilimo nchini Tanzania  (TCCIA) Paul Faraji Koyi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika  Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki  katika wiki ya viwanda mwaka 2021 ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa Julias Nyerere jijini Dar es salaam  

Rais wa CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo  nchini Kenya Richard Ngatia wakati akizungumza na waandishi wa habari katika  Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki  katika wiki ya viwanda mwaka 2021 ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa Julias Nyerere jijini Dar es salaam  

........................................................... 

NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM  

Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuzingatia ukweli na maadili ili kukuza mazingira mazuri ya biashara zao. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Profesa Kitila Mkumbo wakati akifungua Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki  katika wiki ya viwanda mwaka 2021 lenye lengo la kujadili sekta ya viwanda na Biashara baina ya nchi hizo. 

Pro.Mkumbo amesema mafanikio hayo yanatokana na ziara ambayo aliifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan nchini Kenya na hivyo wakuu hao kujadili namna ya kuweka mazingira wezeshi ya biashara.

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda nchini Kenya David Osian amesema uaminifu ndio sababu ya kupiga hatua sekta ya biashara kwa nchi hizo hivyo wanataka kuwe na uzalishaji hivyo Kama nchinya Kenya watahakikisha wanaendelea kukuza bishara sambamba na kwenda katika soko huru la Afrika kwa umoja.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Biashara, Viwanda na Kilimo nchini Tanzania  (TCCIA) Paul Faraji Koyi pamoja  Rais wa CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo  nchini Kenya Richard Ngatia wamesema watahakikisha wanashirikiana kwa pamoja ili kutoa mafanikio katika sekta hiyo. 

Hata hivyo imeelezwa baada ya Kikao cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata imesaidia kuongezeka kwa sekta ya biashara mara sita baina ya nchi hizo mbili hivyo lengo ni kuhakikisha Afrika Mashariki zinafanyika kwa kuzingatia ueledi wa biashara.

 

0/Post a Comment/Comments