ASKARI 11 WALIOPAMBANA KATIKA TUKIO LA KIGAIDI WATUNUKIWA ZAWADI.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro Muliro 
....................................................................

NA MUSSA KHALID

Askari 11 waliopambana katika tukio la Kigaidi la Hamza Mohammed wametunukiwa na jeshi la polisi hati ya ujasiri na fedha kwa kila mmoja kama chachu ya mapambano dhidi ya uhalifu mkoani humo.

Hayo  yamejiri  katika hafla ya kuwatunuku vyeti vya ujasiri na kitita cha shilingi laki tano askari polisi 11 walioshiriki kumdhibiti gaidi jijini Dar es Salaam katika tukio lililotokea   Agosti 25 mwaka huu Mtaa wa Kenyatta karibu na ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro Muliro amesema kuwa vita dhidi ya uhalifu mkoani humo ni endelevu na kuwa vyeti hivyo ni chachu ya mapambano dhidi ya uhalifu mkoani humo.

Aidha kamanda huyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kuwafichua wahalifu mkoani humo na kuahidi zawadi ya kiasi cha shilingi milioni 2 itatolewa kwa yeyote atakayefichua uhalifu kwa jeshi hilo.

Aidha miongoni mwa askari polisi waliotunukiwa vyeti hivyo amesema kuwa kazi ya jeshi hilo ni kulinda usalama wa taifa ambapo amewaasa askari kufanya kazi kwa moyo wa uzalendo kulinda usalama wa raia na mali zao.

Kamanda Muliro Jumanne Muliro amewaasa wananchi kuacha kubeza kazi ya jeshi la polisi kwani wapo kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

0/Post a Comment/Comments