........................................................
Na
mwandishi wetu Dodoma
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais ,Muungano na Mazingira Seleman Jafo amesema
nchi ya Tanzania kuendelea kuwa kisima cha Amani Duniani ni kutokana na
mshikamano mkubwa wa viongozi wa Dini kuendelea kuliombea taifa.
Waziri
Jafo amebainisha hayo leo Septemba 21,2021 jijini Dodoma katika kongamano
la kitaifa la Amani ambalo limekwenda sambamba na maadhmisho ya
amani Duniani.
Waziri
Jafo amesema amani inaweza ikatoweka kutokana na masuala mbalimbali
ikiwemo majanga ya asili ikiwemo matetemeko ya ardhi,magonjwa,uonevu,utawala
usiofuata sheria na uonevu lakini Tanzania imekuwa nchi ya kuigwa kwa
kustahimili amani hivyo ni kutokana na viongozi wa dini kuwa mstari
wa mbele kuliombea taifa na kuhamasisha waumini kutunza amani.
Hivyo,Waziri
Jafo amewataka watanzania kuendelea kulinda amani kuanzia ngazi ya familia na
kukemea viashiria vya uvunjifu wa amani.
Mwakilishi
mkaazi ,Umoja wa mataifa[UN ],Zlatan Millisic amesema ,wao kama Umoja wa
Mataifa wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha kama ilivyo malengo endelevu lengo
namba 16 la Umoja wa Mataifa huku akipongeza serikali ya Tanzania
kwa kuendelea kulinda amani.
Nao baadhi ya wadau wa amani
nchini wakiwemo wananchi na viongozi wa asasi mbalimbali za kiraia wamesema
amani ni msingi muhimu kwa maendeleo ngazi ya familia mpaka Taifa.

Post a Comment