Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi
Profesa Makame
Mbarawa (picha na mtandao)
.............................................................
NA
SALYM BITCHUKA
Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi
Profesa Makame
Mbarawa amemtaka mkandarasi anayejenga
barabara ya mwendo
kasi (BRT) ya
Mbagala Mision kurudia
ujenzi wa barabara
hiyo yenye ukubwa
wa kilomita mbili
kutokana na kukosa
viwango bora vya
ujenzi.
Waziri Mbarawa
ameyasema hayo leo jijini
Dar es Salaam akiwa
kwenye ziara ya kukagua
miradi ya barabara za BRT
, Njia nane na
Kituo cha Kipya cha Mabasi cha Mbagala .
Aidha Profesa
Mbarawa amesema kipande
cha barabara ya Mbagala
Mission kimeanza kuonyesha
mipasuko kabla ya
matumimizi kitendo kinachoonyesha kukosa
viwango bora vya ujenzi
huku akitoa miezi
Mitano kwa Mkandarasi
kuirudia barabara hiyo yenye
ukubwa wa kilomita
mbili kwa gharama
zake.
Aidha waziri
Mbarawa ameahidi kuanza
kutumia teknolojia mpya
ya kukagua ubora
wa barabara huku akitoa Maelekezo
kwa wasimamizi wa Barabara
nchini TANRODS Kufika Ofisi
za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
kupatiwa mtambo utakaowezesha
kuondokana na barabara
sizizo na ubora.
Kwa upande
wake Mtendaji mkuu
wa TANRODS Mhandisi Rogatus
Hussein Mativila akizungumzia
mapungufu yaliyoonekana katika
barabara BRT Mbagala amesema
yametokana na Mkandarasi wa
ujenzi huo kutumia
mchanga usiofaa katika
ujenzi .
Mradi huo wa
ujenzi wa babarabara BRT wenye thamani
ya Shilingi Bilioni 217 ulianza
Desemba 10, 2018 na ulitarajiwa
kukamilika mwaka huu 2021 lakini kwa
sasa unatarajiwa kukamilika March 2023 kutokana
na matatizo yaliyokuwepo awali katika
utawala.

Post a Comment