......................................Serikali ya Ujerumani imeahidi kuendelea kushirikiana na Makumbusho ya Taifa katika nyanja ya Utafiti,maonesho, kubadilishana uzoefu na program mbalimbali ili kuendeleza uhifadhi wa urithi wa kihistoria, Mambokale na utamaduni kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa baada ya kikao maalum na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani Robert Doelger alie ambatana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Mhe. Regine Hess kwa lengo la kuyatazama mashirikiano ya sasa na kuona fursa zaidi za mashirikiano mengine.
Mkurugenzi huyo wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani Robert Doelger na Balozi Hess walipata nafasi ya kutembelea maonesho mbalimbali pamoja na fuvu la binadamu wa kale anaesadikika kuishi miaka Milioni 1 laki saba iliyopita Zinjanthropus
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Program Makumbusho ya Taifa Chance Ezekiel anabainisha faida watakayo ipata kwa upande wa program za kimakumbusho hasa zinazohusu Sanaa na Utamaduni.
Aidha Watanzania wametakiwa kuwa na muamko wa kujiwekea mazoea ya
kutembelea Makumbusho ili kujifunza mambo yahusuyo utalii wa ndani na kufahamu
fursa mbalimbali zilizowahi kuwepo na ambazo zipo ndani ya nchi.
Post a Comment