WATANZANIA WAENDELEA KUKUMBUSHWA KUJIHADHARI NA UVIKO 19

Viongozi wa Dini mbalimbali walipokuwa wakiwasha mishumaa kuashiria amani

.......................................................................

NA MUSSA KHALID

Katika kuadhimisha siku ya amani Duniani Watanzania wametakiwa kuendelea kujikinga na kujihadhari na ugonjwa wa UVIKO 19 ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwa wingi  kuchanja ili kuweza kukabiliana na maradhi hayo.

Hayo yamejiri Septemba 21 jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani ambayo yameadhimishwa katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambapo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini.

Akizungumza katika Hafla hiyo Mgeni Rasmi ambaye ni Mwakilishi  kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa UNFPA nchini Tanzania Jacqueline Mahon amesema maadhimisho ya mwaka huu yanakwenda sambamba na kauli isemayo Kupona vizuri kwa ajili ya Dunia ya usawa wa haki na iliyoendelevu’ lakini pia dhumuni kukumbusha wananchi kujihadhari na UVIKO 19.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Elifas Bisanda amesema ili watanzania kuendelea kuidumisha amani ni vyema wakaendelea kujitokeza kwa wingi kwenda kuchanja ili waweze kuishi kwa usalama zaidi.

Kwa upande wake Mtafiti Mkuu kiongozi wa Magonjwa ya Binadamu katika Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO  nchini Tanzania  Profesa Hamis Malebo amesema ili kukabiliana na ugonjwa huo amegundua Dawa ya COVIDO ambayo imesaidia kuleta matokeo mazuri ndani ya masaa 24.

Maadhimisho ya amani duniani huadhimishwa kila ifikapo septemba 21 ya kila mwaka ambapo mwaka huu yanakwenda sambamba na kaulimbiu isemayo,”Kujikwamua vyema Zaidi kwa ulimwengu wenye usawa endelevu.

0/Post a Comment/Comments