ZIC YADHIMIRIA KUWAUNGA MKONO WANAWAKE WAJASIRIAMALI MKOANI MTWARA.

 


   Mkurugenzi wa wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya pichani akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la bima Zanzibar (ZIC) Arafat Haji pamoja na wawakilishi wengine kutoka Shirika Hilo Mara baada ya kukutana na kujadili Tamasha la wanawake wajasiriamali mkoani Mtwara ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 19 mwaka huu Mkoani Mtwara.


  Na.Khadija Seif, Michuzi Tv


SHIRIKA la bima la Zanzibar (ZIC) wadhamiria kujitolea Kudhamini Tamasha la wajasiriamali wanawake Mkoani Mtwara linalotarajiwa kufanyika mapema septemba 19  mwaka huu Mkoani Mtwara.


Akizungumza na Michuzi Tv , Mkurugenzi wa shirika hilo Arafat Haji Mara baada ya kukutana na Mkuu wa wilaya ya Mtwara  Dunstan Kyobya nakuzungumza mengi  amesema kwa mara nyingi shirika hilo limekua likitoa huduma katika Mkoa huo hivyo ni wakati wa kurejesha kwa wateja wao.


"Tulikua tunatoa huduma zetu hapa Mtwara hivyo tuna njia nyingi za kurejesha kwa jamii hususani wateja wetu na hata wasio wateja wetu na tumehaidi kuwepo katika Tamasha la wajasiriamali wanawake ambapo kimsimgi kuwaunga Mkono wanawake hao."


Hata hivyo Haji ameeleza kuwa katika Tamasha Hilo wataweza kutoa Elimu kwa wanawake hao wajasiriamali kwa namna gani wataweza kujilinda na kutumia bima kwa maslahi ya familia zao pamoja na Biashara zao kwa ujumla.




.... Mwisho...

0/Post a Comment/Comments