Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es salam ACP Muliro Jumanne Muliro
...................
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limesema linafanya uchunguzi juu ya tukio linalodaiwa kuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Zimbili iliyopo Kinyerezi Wilaya ya Ilala (jina linahifadhiwa) ambaye amemuadhibu kwa viboko kupita kiasi mwanafunzi aitwaye Swaumu Hussein miaka 9, anayesoma darasa la tatu ambaye baadaye alipoteza maisha.
Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es salam ACP Muliro Jumanne Muliro ametoa taarifa hiyo leo kwa vyombo vya habari na kusema tukio hilo lilitokea tarehe 18/10/2021 huko Wilaya ya Ilala katika Shule ya Msingi Zimbili Kinyerezi iliyopo Ilala.
Amsema Uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo unafanyika ili kubaini chanzo halisi cha kifo hicho na mifumo ya kisheria itatumika na kuzingatiwa wakati wa uchunguzi
Post a Comment