Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Geoffrey Mwambe (kulia) Pamoja na Raisi wa Jumuiya ya Muungano Kimataifa chini ya kundi la Afrika na Asia (Afro- Asian union (AFASU) Dr. Hossam Darwish (kuchoto) wakitia saini ya hati ya makubaliano ya Ushirikiano
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Mhe. Geoffrey Mwambe Pamoja na Raisi wa Jumuiya ya Muungano Kimataifa chini ya
kundi la Afrika na Asia (Afro- Asian union (AFASU) Dr. Hossam Darwish wametia
saini hati ya makubaliano ya Ushirikiano kuwezesha kukuza na kuunda
ushirikiano katika sekta ya uwekezaji , wenye lengo la kuwezesha na
kukuza uwekezaji, biashara na utalii nchini Tanzania .
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini
makubaliano hayo iliyofanyika katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Jijini Dar es
salaam, Mhe. Mwambe ameainisha maeneo ambayo Tanzania na ASAFU watashirikiana
katika kuvutia maeneo ya uwekezaji kuwa ni pamoja na uwekezaji katika
Afya,kilimo, Viwanda, Biashara Mtandao, Utalii, Elimu pamoja na Uwekezaji
katika TEHAMA.
Mhe. Mwambe ameeleza kuwa kusainiwa kwa
hati ya makubaliano kunaonyesha dhamira kubwa ya serikali ya awamu ya
sita ya kushirikiana na wadau wote duniani na kuwaalika
katika uwekezaji lakini pia kutumia fursa ya kuaminika kama
serikali ya Tanzania kuweza kuwaomba Taasisi na sekta binafsi
waweze kutusemea ili kushawishiana kuja kuwekeza Tanzania kwasababu ya
mazingira bora ya uwekezaji yaliyowekwa nchini.
“Serikali ya awamu ya sita
inaaminika na mazingira ya uwekezaji Tanzania yameendelea
kuboreshwa na pia sisi kwenye Nyanja za kimataifa tafsiri
yake ni kuwa tanzania inaendelea kusifika kwenye ubora wake wa
mazingira ya uwekezaji”Amesema Mhe. Mwambe
Aidha Mwambe amewashukuru wawekezaji hao
na kuwahakikishia kuwa ofisi yake iko tayari kushirikiana nao kwa kuweka
mazingira wezeshi ili kuhakikisha wanafanikiwa, na kuwataka watanzania na
Taasisi nyingine za serikali kuwapa ushirikiano wa kutosha ili waweze
kufanikiwa kuwekeza nchini.
“Nawashukuru sana AFASU, nawakaribisha
sana na ninawaomba watanzania tuendelee kuwapa ushirikiano wote pale
ambapo wataitaji vibali, ardhi, na idhini mbalimbali za serikali
ili waweze kutekeleza mradi wao tutahakikisha kwamba tunasimamia
hilo kwahiyo tusingependa kuwakwamisha kwa sababu hii inatupa sifa
sisi na inampa pia amani Mhe. Rais na kuendelea kujenga imani kubwa
kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya hiyo,
Dkt. Hossam Darwish amesema Jumuiya ya AFASU wako tayari kutekeleza vipengele
vyote ambavyo vimo ndani ya makubaliano hayo na watatekeleza kwa
nguvu kubwa na haswa kwa kuanza na sekta ya kilimo ambapo ndani ya
Jumuiya wanao wajumbe ambao ni wawekezaji wakubwa
kwenye sekta ya kilimo ambapo wameona maeneo ya kilimo na
wamevutiwa sana na fursa hiyo ya kilimo hapa nchini na hivyo
wanatoa ishara njema kwamba wao watakuwa ni sehemu ya uwekezaji katika
sekta hii ya kilimo pamoja na sekta nyingine ambazo zitakuwa zimeainishwa
katika makubaliano.
Dkt. Hossam ameongeza kuwa kwa
hatua ya kwanza na kwa haraka wataanza na mradi wa chuo cha
Kimataifa cha Kitanzania cha mifumo ya kielektroniki ambacho kitakuwa na
vitivo vitivo 14 vya kimasomo ya kielimu na wanaimani kwamba vitivo
hivyo vinaweza kwenda sambamba na kile walichokiona kinahitajika
ndani ya nchi yetu ambapo shahada mbalimbali zitatolewa kupitia
chuo hicho na kitaweza kuchukua wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za Afrika na
nje ya Afrika, nakuhakikisha kuwa mfumo wa masomo utaweza kutoa wataalamu wa
kutosha.
Amesema hatua nyingine itakayofuata ni mradi wa maonyesho ya biashara
ambayo yatafanyika hapa nchini Tanzania ili kuweza kuchochea uwekezaji na pia
jumuiya hiyo itajikita katika uwekezaji wa masuala ya utalii hususan katika
ujenzi wa hoteli zenye hadhi kubwa na katika sekta ya afya watajikita katika
ujenzi wa viwanda vya kuzalisha Dawa na vifaa Tiba .
Kwa upande mwingine Dkt. Hossam
amemshukuru Waziri wa Uwekezaji kwa kuonesha uzalendo mkubwa kwa nchi
yake ambapo amekuwa na juhudi kubwa sana na kwa upande wake anamatumaini
makubwa kuwa Tanzania itapiga hatua katika sekta hii ya uwekezaji kwa juhudi
kubwa ambazo anazifanya Waziri wa Uwekezaji.
Hafla hiyo ya utiaji Saini wa hati ya makubaliano ya Ushirikiano
ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji Tanzania, Dkt.
Maduhu Kazi, na Mkurugenzi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TanTrade), Latifa Khamis, pamoja na maafisa wa serikali kutoka Ubalozi
wa Tanzania nchini Misri, Wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki
MWISH
Post a Comment