KAMPUNI ya Cocacola kwanza imekabidhi soko la wafanyabiashara wadogo 100 kwa serikali soko hilo lililopo la Kigogo Dampo ilikusaidia wafanyabiashara wadogo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi soko hilo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewapongeza Cocacola kwanza kwa kuweza kuiungamkono serikali ya Rais Samia.
"Mmejuwa kutufariji wakati wa shida tukiwa tupo kwenye changamoto ya machinga ndio mmeweza kutufikiria na kutupa soko sisi kama serikali tutahakikisha tunalitanua na kuwa kubwa zaidi.
"Ililiweze kuchukuwa wafanyabiashara wengi zaidi tutahakikisha hata magari yanakuja na kuleta watu waweze kununua vitu kwa wafanyabiashara watakaokuwa humu" amesema Makalla
Aidha aliwashukuru kwa kuwa wamekuwa ni watu wanao wakimbilia na kuwasaidia katika kila changamoto waliweza kujenga vibanda Cocobeach na sasa wamejenga soko Kigogo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Coca cola kwanza Unguu Sulay, amesema kuwa waliona ni vizuri kuweza kujenga soko ili kurahisisha wakazi wa kigogo na maeneo ya karibu kupata mahitaji.
Post a Comment