PBZ BENK YAWATAKA WATANZANIA KUTEMBELEA BANDA LAO MNAZI MMOJA NA KUFUNGUA AKAUNTI.


Afisa Mahusiano wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Bank Salim Hassan akizungumza na mwandishi wa blog hii katika katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam

.........................

NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM

Benki ya Watu wa Zanzibar -PBZ Bank imesema licha ya kuwahudumia wateja pia inatoa elimu na ushauri kwa lengo la kusaidia kusogeza huduma za kifedha kwa wateja.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika maonesho ya wiki ya huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam Afisa Mahusiano wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Bank Salim Hassan amesema pamoja na masuala ya elimu ya kifedha pia wanawaelimisha wateja kuweka akiba sambamba na kufungua akaunti.

Salim amesema benki hiyo imekuwa ikijikita kufungua matawi katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha watanzania wanafikiwa na huduma za kifedha kwa ukaribu.

‘Kimantiki hasa tupo kwa ajili ya kushirikiana na baadhi ya taasisi ambazo zinafanana na zakwetu katika kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa watanzania na hapa mnazi mmoja tunazofursa za kuwaeleza kwa undani zaidi kuhusiana na fursa zetu za kimikopo’amesema .’amesema Salim

Aidha Afisa Mahusiano huyo amesema ni vyema watanzani wakaitafuta pesa lakini pia kufahamu namna ya kuitunza na kuiendeleza kwa kuwa na akauti benk.

‘Tunalenga kuwashauri wateja wetu wafungue zile akaunti ambazo wakiziweka kwetu sisi tutaweza kuizungusha ile pesa na faida kitakachopatikana tutaweza kukigawa maana yake mteja wetu aweze kupata fungu kupitia huduma ya Fixed Accout’amesema Salim

Hata hivyo amesema PBZ Benk wanaendesha katika mifumo miwili ya kihuduma ukiwemo wa kawaida pamoja na mfumo wa Kiislamu ambao hauhusishi Riba.

0/Post a Comment/Comments