NAIBU WAZIRI SILINDE AUAGIZA UONGOZI WA MKOA WA MOROGORO KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO





Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde ameagiza uongozi wa Halmashauli za Wilaya katika mkoa wa Morogoro ambazo bado wapo nyuma katika ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kuhakikisha wanasimamia kwa karibu zaidi mafundi waweze kukamilisha kwa wakati kama mda ulivyoongezwa na serikali wa tarehe 30 December 2021 ili kuruhusu wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza kuanza kutumia madarasa hayo.

Ametoa maagizo hayo akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri nne za mkoa wa Morogoro ambazo ni Gairo,kilosa,Mvomero na Manispaa ya Morogoro na kukuta ni halmashauri moja tu ya kilosa ndiyo iliyomaliza ujenzi kwa asilimia mia huku halmashauri ya Gairo ikiwa bado ipo nyuma wakiwa wanaezeka mabati katika majengo yao yote waliyopewa na kutaka waongeze spidi kwa kufanya kazi usiku na mchana kwani mda uliongezwa ni mdogo kuliko kazi ambazo bado wapo nazo.

Aliongeza kuwa ametembelea halmashauri ambazo zipo mbali sana na viwanda vya cement zinapozalishwa na vifaa vingine kama Katavi Rukwa,Songwe lakini wamekamilisha majengo yao lakini inashangaza  kuona mkoa wa Morogoro ambao upo karibu na viwanda vya uzalishaji wa vifaa bado upo nyuma kukamilisha kwa uharaka ujenzi wa madarasa na kutaka wakamilishe kwa wakati ikiwezekana kabla ya tarehe ya mwisho kwa ubora na thamani halisi ya fedha zionekane.

Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Morogoro Marium Mtunguja amesema sababu kubwa ya halmashauri ya Gairo kua nyuma katika ujenzi wa madarasa ni kutokana na kuagiza cement Tanga ambapo walikuta foleni kubwa ya utaji wa bidhaa hivyo kufanya kuchelewa lakini wanaamini ndani ya mda uliongezwa watakamilisha kwa wakati na halmashauri zingine ambazo nao wanakamilisha ujenzi huo 

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga amemahukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa vyumba vya madarasa ambavyo sasa vitasaidia kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika chumba kimoja ambao walikua wanawaweka mpaka wanafunzi 100 kwa wakati mmoja lakini sasa watakaa wanafunzi 45 tu hivyo kufanya ufaulu kuongezeka.

0/Post a Comment/Comments