TAASISI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE INATALAJIA KUFANYA KUMBUKUZI YA MIAKA 100 YA KUZALIWA KWA BABA WA TAIFA MKOANI MARA.

 TAASISI YA  KUMBUKUMBU YA MWALIMU JULIUS KAMBARANGE NYERERE INATALAJIA KUFANYA KUMBUKUZI YA MIAKA   100 YA KUZALIWA KWA BABA WA TAIFA MKOANI MARA.    


Mwenyekiti wa wa taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu JULIUS KAMBARANGE NYERERE wa kwanza kushoto akimkabidhi kadi ya uanchama Mwandishi wa habari wa icon media Bwana Richard Mrusha.



Wa kwanza kushoto mwenyekiti wa wa taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu JULIUS KAMBARANGE NYERERE Paul Kimiti akimkabidhi kadi ya uanchama Mwandishi wa habari wa global tv Ndugu Denisi Mtima.


Mwenyekiti wa wa taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu JULIUS KAMBARANGE NYERERE Paul Kimiti akizungumza na waandishi wa habari


Na Richard Mrusha


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Paul Kimiti, amesema lengo la kufanya kumbukizi hiyo na  makongamano Sambamba na ziara hiyo ni kuenzi na kutambua mchango uliofanywa na Baba wa Taifa enzi za uhai wake.


Amesema makongamano hayo ya  kuelekea kumbukumbu ya miaka 100 ya Mwalimu Nyerere yatahusisha kanda sita ikiwemo ya ziwa Victoria Kanda  Kasikazini (Arusha), Kanda ya Kati (Dodoma) Kanda ya nyanja za juu Kusini (Iringa) 


Alizitaja Kanda nyingine ni Magharibi (Katavi) na Kanda ya Kusini (Lindi) na Mtwara na baadae Mkoa wa Dar es Salaam na visiwani Zanzibar.


Amesisitiza kuwa mbali na mada zitakazotolewa pia kutakuwa na matukio ya upandaji wa miti kabla ya kufanyika kwa  makongamano hayo ambayo kimsingi yataudhuriwa na watu wa kada mbalimbali.


Kimiti ameongeza kwamba maeneo yote ambapo Taasisi hiyo itafanya makongamano, yana historia na kumbukumbu ya matukio mbalimbali ya kitaifa yaliyowahi kufanywa na Hayati Baba wa Taifa enzi za uhai wake.


Kwa mujibu wa Kimiti siku rasmi yatakapofanyika maadhimisho ya miaka 100 ya Baba wa Taifa ni mwezi wa nne 13, mwaka huu 2022 uko mkoani mara alikozaliwa  hayati JULIUS KAMBARANGE NYERERE.


Na Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Taasisi hiyo, Balozi Francis Mndolwa, amesema dhamira yao ni kuifanya taasisi hiyo kuwa na misingi imara na endelevu.


Amesema kwamba, kupitia taasisi hiyo Watanzania watapata historia, falsafa na itikadi zilizoasisiwa na Baba wa taifa na kuziishi kwa maslahi ya amani na utulivu katika kipindi cha miaka 60 ijayo.


Aidha ameongeza kwamba taasisi hiyo haifungamani na chama chochote Cha siasa hivyo watu wote wanatakiwa kujiunga kwenye taasisi hiyo ili kuweza kuyaenzi yale mema aliyoyafanya hayati JULIUS KAMBARANGE NYERERE enzi za uhai wake.


Na kupitia hafla hiyo Kuna waandishi wa habari wawili wameweza kujiunga kwenye taasisi hiyo kwa kukata kadi ambayo inalipiwa kiasi Cha fedha ya kitanzania sh 5000 na kuweza kuwa mwanachama, waandishi hao ni Denisi Mtima wa global tv na Richard Mrusha wa icon media.

0/Post a Comment/Comments