Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha waliofika kumpokea wakati akitokea nchini Marekani
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Arusha, kuzindua Filamu ya Royal Tour inayotangaza vivutio vya Utalii,Utamaduni na fursa za Uwekezaji nchini Tanzania.
Katika Filamu hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan ametumia muda mwingi kuelezea fursa za Utalii na Uwekezaji zilizopo Tanzania akiwa mwongoza watalii namba moja.
Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro Rais Samia Suluhu Hassan amepokewa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Balozi Dkt Pindi Chana, Mawaziri, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela, Manaibu Mawaziri, Makatibu Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, viongozi mbalimbali na wananchi.
Katika Salam zake Rais Samia Suluhu Hassan amewashukuru wote walioshiriki kikamilifu katika kufanikisha kurekodiwa kwa Filamu hiyo na kuwashauri watanzania wachangamkie furusa zitakazo tokana na matokeo chanya ya Filamu hiyo.






Post a Comment