Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe Anisa Mbega akifungua Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India Jijini Chennai, India. |
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kongamano hilo. .......................... Imeelezwa kuwa
zaidi ya wafanyabiashara na wawekezaji 110 kutoka Nchini Tanzania na India
wamehudhuria kongamano la biashara na uwekezaji (Tanzania India Trade
Conference katika jiji la Chennai India. Kongamano hilo
limesaidia kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi hizo mbili
kukutana na taasisi zinazohusika na maswala ya uwekezaji na biashara nchini
kama vile Kituo cha uwekezaji nchini –TIC, Mamlaka ya maendeleo ya biashara
–TANTRADE na mamlaka ya mapato nchini –TRA. Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa kongamano hilo, Balozi wa Tanzania nchini India Mhe, Anisa Mbega
ambapo amesema mataifa hayo mawili yanahistoria ya muda mrefu ikiwa ni pamoja
na mahusino ya kidiplomasia. “Tanzania na India ni
marafiki na Nchi hizi zimekuwa na mahusiano mazuri ya kidiplomasia kwa muda
mrefu ambayo yamejenga msingi imara katika biashara na uwekezaji kati ya nchi
hizo”. Balozi Anisa amesema Amesema Lengo la
Kongamano hilo lilikuwa kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana
nchini Tanzania kwa wafanyabishara na wawekezaji waliopo nchini India. Aidha, ameongeza kuwa
India ni nchi muhimu kwa Tanzania kwani ni nchi ya tano kwa uwekezaji na
biashara nchini Tanzania ambapo wawekezaji kutoka India wamewekeza mtaji wa
kiasi cha dola za Marekani Bilioni 3.7. Aidha, wafanyabiashara
wa India walioshiriki Kongamano wameonesha nia ya kushiriki maonesho ya 46 ya
biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam ambayo yataanza tarehe 28 Juni hadi
tarehe 13 Julai, 2022 ambapo watakutana na wafanyabiashara na kuona bidhaa zinazozalishwa
nchini Tanzania. Kongamano hilo
limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na taasisi ya
Uchumi na Biashara ya India (Indian Economic Trade Organization) huku
likhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya India kutoka Wizara ya Mambo
ya Nje na Wizara inayosimamia masuala ya biashara na wajasiriamali na viongozi
wa serikali kutoka Jimbo la Tamil Nadu lenye makao yake makuu Jijini Chennai.
|
.jpg)

Post a Comment