BIASHARA YA SHISHA KOSA LA JINAI

 



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, ametoa miezi miwili  kwa TMDA kushirikiana na Tume ya dawa za kulevya nchini kufanya  utafiti wa shisha kuwekwa dawa za kulevya.

Waziri Ummy amesema maelekezo yake ni kufanya tathimini ya bidhaa hizi, ili kulinda afya za jamii kwani kufanya biashara ya shisha ni kosa la jinai.

“Sheria ya kudhibiti matumizi ya bidhaa za tumbaku nchini sura ya 121, haijatekelezwa kikamilifu, TMDA mfanye tathimini kwa kina". Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

0/Post a Comment/Comments