NA
SALYM BITCHUKA
Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesema, kampuni za usafiri kwa njia ya
mtandao Bolt na Uber zinatarajia
kurejea kutoa huduma za usafiri nchini Tanzania.
Hayo
yamesemwa leo Jumatatu, Septemba 12, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu
Suluo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Latra
wametoa taarifa hizo kipindi ambacho kampuni hizo kwa nyakati tofauti,
walisitisha kutoa huduma za usafiri za magari na kubaki na bodaboda pamoja na
bajaji.
Suluo
amesema wamesikia kilio cha kampuni hizo na wameitana kukaa meza moja kwa
mazungumzo na tayari wamekubaliana kutatua tatizo ili kurejesha huduma.
"Uber
walijitoa baada ya tangazo la Latra la nauli na tiketi za mtandao ambao
uliwataka kutoza tozo haalali kwa amri ya kutekelezwa na wakafungua kesi Baraza
la Ushindani kupinga maamuzi yetu.”
“..Bolt
waliendelea kutoa huduma lakini baadae nao wakaleta taarifa kuwa wanaenda
kusitisha huduma lakini tuliwaita tukiamini katika mazungumzo" amesema
Suluo
"Tuliwaita wakaja na wawakilishi wao wa Afrika, tukaanza Septemba 5-8, 2022 tumemaliza mazungumzo ambapo kuna taarifa tunataka watuletee kimaandishi ili kutoa maamuzi na leo ndio mwisho wa mda tuliokubaliana na tutatoa maamuzi yatakayowasaidia wote wakiwemo umoja wa madereva teksi (TODA)," amesema mkurugenzi

Post a Comment