Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe Adam Malima wamemtembelea Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Pius Msekwa na mke wake Mama Anna Abdallah katika makazi yao Kisiwani Ukerewe.
Waziri Ummy amesema kuwa ziara yake hiyo imelenga kuja kukagua ujenzi wa miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ukerewe kufuatia kuwepo kwa mgogoro katika ujenzi wa Hospitali hiyo pamoja na kuchunguza ubadhirifu wa fedha.
Kwa upande wake Mzee Pius Msekwa amempongeza Waziri Ummy kwa uchapakazi pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusogeza karibu huduma za matibabu kwa wananchi na kushauri hatua zichukuliwe kwa wale wote wanaohujumu jitihada za Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi.



Post a Comment