BILIONI 50.2 KUING'ARISHA B'MULO


Mwenyekiti wa halmashauri ya B'mulo, Leo Rushau,akitoa maagizo ya baraza.
Diwani wa kata ya Kalenge,Erick Method,akichangia hoja ya mapato kwenye baraza hilo.
Ofisa mipango,Shangwe akiwasilisha makadilio ya bajeti kwenye kikoa cha madiwani Biharamulo.

Madiwani wakiendelea kusikiliza kwa kina mapitio ya bajeti ya halmashauri hiyo.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Daniel Limbe,Biharamulo

HALMASHAURI ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 50.2 bilioni katika bajeti ya mwaka 2023/24 ukilinganisha na 44.1 bilioni iliyokisiwa kwa bajeti ya mwaka 2022/23 kitendo kinachotafsiliwa kuwa fedha hizo zitaing'alisha halmashauri hiyo.

Kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika mwaka huu 2023 ambapo fedha hizo zinatarajiwa kupatikana kupitia ruzuku kutoka serikali kuu,vyanzo vya ndani vya halmashauri,wadau wa maendeleo na wahisani mbalimbali.

Akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa bajeti ya mwaka 2023/24 kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo,kwenye kikao baraza la madiwani, Ofisa mipango, Shangwe Kabuye, amesema upatikanaji wa fedha hizo utachocheo kasi ya maendeleo ya wilaya hiyo.

Amesema fedha hizo zitaelekezwa kwenye kulipa mishahara ya watumishi,utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi,pamoja na matumizi ya kawaida huku bajeti hiyo ikiwa na ongezeko la aslimia 12 ukilinganisha na bajeti ya mwaka jana.

Kadhalika Kabuye amefafanua kuwa wanatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 3,889,567,645 kama mapato ya ndani, matumizi ya kawaida 884,681,000, mishahara 32,972,686,000 na miradi ya maendeleo ni 12,783,113,000 na kwamba kupitia bajeti hiyo ni hakika kuwa halmashauri hiyo itaendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo.

Mbali na madiwani hao kujadili mapitio ya bajeti iliyomalizika, wameonekana kukerwa na baadhi ya mawakala wa ukusanyaji mapato ya halmashauri hiyo kushindwa kutimiza wajibu wao kama walivyokubaliana kwenye mikataba na kwamba wamekuwa chanzo cha baadhi ya watu kutorosha mapato.

Imeelezwa kuwa baadhi ya magari yenye shehena ya mizigo na mazao yamekuwa yakikwepa kulipa ushuru na baadhi ya wafanyabiashara kupita njia za panya ili wasitozwe jambo linaloweka kusababisha kutofikiwa makisanyo tarajiwa.

Kutokana na hali hiyo,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Leo Rushau,akatoa agizo kwa mkurugenzi wa halmashauri yake kuhakikisha ukusanyaji mapato kipitia mfumo wa POS ufanyike kupitia mawakala wanaoishi kwenye vijiji husika badala ya kuchukua watu kutoka nje ya kata husika kwa kuwa baadhi yao wanahujumu mapato ili waweze kujikimu kwenye maeneo ya ugenini.

"Naagiza siku tatu kuanzia leo wale mawakala wote wanaolalamikiwa kule Nyakanazi waondolewe...maana mimi mwenyewe nilishuhudia gari linapita pasipo kutozwa ushuru hii haiwezekani inaonekana kuna uzembe mkubwa unafanyika kwa hawa mawakala wetu" amesema Rushau.

0/Post a Comment/Comments