Na Shamimu Nyaki
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.
Pauline Gekul amesema Serikali imekuwa ikitoa haki sawa ya ushiriki
katika michezo kwa makundi yote ikiwemo watu wenye ulemavu.
Mhe. Gekul ameyasema hayo Februari 03, 2023
bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Khadija Shaaban (Viti
Maalum) aliyeuliza Serikali ina mkakati gani wa kuinua ushiriki wa watu
wenye ulemavu katika michezo ikiwemo mpira wa miguu, wavu na pete.
"Moja ya mikakati ya Serikali katika kuinua
ushiriki wa michezo kwa watu wenye ulemavu hususani mpira wa miguu, wavu na
pete ni pamoja na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kushirikisha watu wenye
ulemavu katika matukio yote, kusajili Vyama na Vilabu vya michezo kwa
watu wenye ulemavu hususani inayoandaliwa na Serikali," ameeleza Mhe.
Gekul.
Mhe. Gekul ameongeza kuwa Serikali imeendelea
kuziwezesha timu za Taifa za watu wenye ulemavu zinaposhiriki katika mashindano
mbalimbali ya kimataifa.
Aidha, Mhe. Naibu Waziri Gekul amesema kuwa
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo imeendelea kuhamasisha ujenzi wa
miundombinu ya michezo yenye mazingira rafiki kwa walemavu.
Aidha, amevitaka vyama, mashirikisho na vilabu vya
michezo kusajili watu wenye ulemavu na kuwashirikisha katika matukio yote ya
michezo
MHE. GEKUL : SERIKALI INATOA HAKI SAWA USHIRIKI WA MICHEZO
..............

Post a Comment