Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia - Dkt Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Taasisi hiyo kwenye Mkutano wa siku ya uwekezaji na ufunguzi rasmi wa dirisha la kupokea maombi ya ushiriki wa programu ya iMBEJU ya Benki ya CRDB uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu akitembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye Mkutano wa siku ya uwekezaji na ufunguzi rasmi wa dirisha la kupokea maombi ya ushiriki wa programu ya iMBEJU ya Benki ya CRDB uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam
Baadhi ya washiriki ambao wametembelea katika Banda la COSTECH kwenye Mkutano wa siku ya uwekezaji na ufunguzi rasmi wa dirisha la kupokea maombi ya ushiriki wa programu ya iMBEJU ya Benki ya CRDB uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam
Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa kilimo TARI-Mikocheni Margareth Daudi Lupembe akimueleza mdau aliyetembelea katika Banda lao kwenye Mkutano wa siku ya uwekezaji na ufunguzi rasmi wa dirisha la kupokea maombi ya ushiriki wa programu ya iMBEJU ya Benki ya CRDB uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam
.........................
NA MUSSA KHALID
Tume ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH imesema katika suala la uwekezaji inaendelea kuwajengea uwezo vijana kuanza kuwa na mawazo ikiwemo kuweka Mbegu na baadae kuwa wawekezaji.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu amesema hayo Jijini Dar es alaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Taasisi hiyo kwenye Mkutano wa siku ya uwekezaji na ufunguzi rasmi wa dirisha la kupokea maombi ya ushiriki wa programu ya iMBEJU ya Benki ya CRDB uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam ambayo imefunguliwa na Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Dkt Nungu amesema vijana walioshiriki hapo wamesaidiwa na COSTECH kupitia Mfuko wa Taifa wa waendelezaji wabunifu MAKISATE pia kuna watafiti kutokea kituo cha Mikocheni ambao wote wamesaidiwa na Mfuko huo.
"Tunategemea program hii Mpya inaweza ikachukua hasa na kuwekeza mwa sababu mwekezaji yeyote hawezi kuwekeza kwenye wazo kwani lengo Moja ni lazima kuwa na mrejesho hata kama sio Faida Ile Fedha lazima iweze kurejeshwa"amesema Dkt Nungu
Kwa upande wake Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa kilimo TARI-Mikocheni bi. Margareth Daudi Lupembe amesema katika kituo chao kuna mradi wa uzalishaji wa mimea mbalimbali Kwa njia ya chupa hasa mazao ambayo upatikanaji wa Mbegu ni Changamoto.
Amesema kwa sasa kwenye kituo chao kuna mradi wa mananasi ambao unafadhiliwa na COSTECH ambapo yanazalisha kwa njia ya chupa na tayari wameshayapanda katika mikoa mbalimbali ambayo onapanda mananasi ukiwemo Pwani,Morogoro Pamoja na Njombe.
Naye Mmoja wa Wabunifu ambaye anafadhiliwa na COSTECH chini ya DTBi Geoffrey Tenganamba ameeleza Mfumo wa Mazao hub ambao wamekuwa wakiutumia kuwa unasaidia kuonyesha mpangilio mbalimbali ya shamba Pamoja na Bajeti ya kilimo
COSTECH imeshiriki katika Mkutano huo ikiwa ni kuendeleza makubaliano waliyoingia kupitia hati ya makubaliano iliyosainiwa tarehe 20 Februari 2023 ili kuruhusu mchango wa sekta binafsi za kifedha na CRDB kupitia mpango wezeshi wa IMBEJU unaolenga kuwezesha vijana na wanawake kuwapatia mitaji ya ubunifu
Pia Taasisi hiyo imeshiriki kama mtaalamu wa (technical support) ya kufanyia tathimini ya maombi ya wabunifu ili kuwakabidhi wabunifu kwa benki ya biashara ya CRDB





Post a Comment