**********
MSHABIKI mwandamizi wa timu ya mabingwa wa kihistoria wa Klabu ya Yanga, Mzee mpili,amelamba ubalozi wa Kampuni inayojihusisha na uuzaji wa vifaa bora vya magari ya Dar Quality Motors.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Afisa masoko wa kampuni Dar Quality Motors, Shamsa Mseremo,wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akimtangaza kuwa balozi wa kampuni hiyo.
Mseremo,amesema amesema wameamua kumpa ubalozi huo kwa sababu anauwezo na anakubalika ndani ya jamii.
"Tunawahakikishia wateja wetu kupitia mzee mpili tutaendelea kutangaza bidhaa zetu bora "Amesema Mseremo,
Hata hivyo,Mseremo kampuni hiyo kwa sasa inasifika kwa uuzaji wa bidhaa bora za magari na tunawataka watanzania wajitokeze kupata huduma zetu.
Huku naxe Balozi wa Kampuni hiyo Mzee Mpili amesema kuwa yupo vizuri na Kampuni hiyo haitajutia kumpa ubalozi huo kwani atazitangaza bidhaa zao kwa uzuri zaidi na kuwasihi watanzania wajitokeze kupata bidhaa hizo.
Pamoja na hayo mzee mpili amesema mkataba wake na Kampuni hiyo upo vizuri na kupitia menejimenti yake itamsimamia ili apate faida na kujiinua kiuchumi.


Post a Comment