**************
BENKI ya (KCB),imesema itaendelea kusaidia jamii hasa makundi maalum ikiwa ni sehemu ya benk hiyo kurudisha kwa jamii kupitia faida wanazozipata.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa mahusiano wa benki hiyo,Christina Manyenye,wakati wa benki hiyo ilipokuwa inatoa msaada wa vyakula kwa kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo kinondoni Hananasif.
Manyenye amesema Benki ya KCB inatambua inapaswa kurudisha kwa jamii hasa kwa watanzania wanaopata shida mbalimbali.
"Benk yetu inatambua umuhimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kufanya mema na kwakutambua umuhimu huo,tumeamua kurudisha kuja kuwasaidia msaada wa Vyakula mbalimbali kwa kituo hiki cha kulea watoto yatima"Amesema Manyenye.
Hata hivyo,Manyenye,amesema sanjari na msaada huo benki ya KCB imeendelea kuwasaidia makundi mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana kutoa veta ili waweze kujiajiri na kuwasaidia watanzania wengine.
Kwa upande Mkuu wa huduma za Benki za kiislamu –KCB Sahl Banking, Amour Muro,amesema benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa watanzania ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Naye,Mkuu wa kituo cha Kulea watoto Yatima cha Maunga Centre,Rashid Matimba,ameishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema msaada huo umekuja wakati muafaka.
"Tunaipongeza benk KCB kwa msaada wao,tunaomba benki zingine waige mfano wa benki hii''Amesema Matimba.


Post a Comment