PROF. MKENDA ATOA RAI KWA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI KUSHIRIKI MAONESHO NA MAADHIMISHO YA WIKI YA UBUNIFU





 ......................

Dodoma: 

Waziri Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolph Mkenda ametoa rai kwa Taasisi za umma na binafsi kushiriki maonesho na maadhimisho ya wiki ya Ubunifu Kimataifa.

Ameyasema hayo  alipokuwa akizungumza wakati wa Mkutano na Vyombo vya habari kuhusiana na Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu yatakayofanyika kuanzia tarehe 24 - 28 Aprili 2023  Kitaifa Uwanja wa Jamhuri - Jijini Dodoma 

Waziri ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), Mhe.  Prof. Adolf Mkenda amesema wizara inaendelea na Maandalizi na kuwaalika Taasisi, Mashirika, Wizara za Kisekta pamoja na wananchi kushiriki Maadhimisho hayo Kitaifa ikiwa ni mkakati wa Serikali kuongeza hamasa ya matumizi ya Sayansi,  Teknolojia na Ubunifu kama nyenzo ya kufikisha maendeleo kwa haraka ya Kiuchumi na Kijamii. 

" Tangu 2019 wizara imekuwa ikishirikiana na wadau wengine ikiandesha Wiki ya Ubunifu na MAKISATU kwa lengo la kuimarisha mfumo wa Ubunifu hapa nchini, Juhudi hizi zimetusaidia kuingiza bunifu mbalimbali  sokoni na nina orodha ya bunifu 38 na mojawapo maarufu zaidi ni ya mita ya maji ambayo imeanza kubiasharishwa" alisema Prof. Mkenda 

Aidha, Prof Mkenda amefafanua kuwa Wiki hii inafanya lengo la kutoa fursa kwa wabunifu wa Kitanzania kujulikana na wawekezaji na  kukutanisha wadau wa sekta mbalimbali kujadili kwa pamoja sera na miongozo ihusuyo maendeleo ya Sayansi,  Teknolojia na Ubunifu na kwa mara ya kwanza safari hii tutakuwa na ushiriki kutoka Afrika ya Kusini, hivyo Maadhinisho yataanza kuchukua Sura ya Kimataifa " 

Vilevile, Mhe. Prof. Mkenda ameongeza kuwa Maadhimisho yatahusisha maonesho ya ubunifu na Teknolojia toka Taasisi za Elimu ya Juu , Taasisi za Utafiti na Maendeleo, Mashirika na Makampuni ya Umma na binafsi,  Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi yani VETA na shule za sekondari na msingi. 

Alihitimisha kuwa Wiki ya Ubunifu Tanzania  itaendeshwa katuka Mikoa 17 ya Tanzania bara na Visiwani kwa ngazi ya Mikoa na Halmashauri na itaratbiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) , programu ya Funguo chini ya usimamizi wa UNDP , Ofisi ya Rais - TAMISEMI na wadau wengine mbalimbali nchini.

0/Post a Comment/Comments