Na PETER CHARLES
Jeshi la Polisi mkoa wa Ilala limewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Ilala.
Hayo yamesemwa 15/04/2023 katika viwanja vya Shule ya msingi Tabata na Mkuu wa Opareheni na mafunzo mkoa wa Ilala ACP ABUBAKARI KUNGA alipomwakilisha Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Dr. Debora Magiligimba katika hafla ya kufunga mashindano ya Polisi Jamii mkoa wa Ilala.
Aidha ACP KUNGA amekabidhi kombe na zawadi ya Tsh. 500,000 kwa timu ya mpira ya Tabata fc ambao ni washindi wa kombe la Polisi Jamii cup mkoa wa ilala baada ya kuwafyatua Kiwalani fc waliopata zawadi ya Tsh. 300,000 katika mikwaju ya penati 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika bila kufungana, huku timu ya Polisi veterani ikishika nafasi ya tatu na kujinyakulia Tsh 200,000 baada ya kuwachabanga Polisi Kati Penati 5-4 baada ya matokeo tasa ndani ya dakika 90.
Kwa upande wake captaini wa timu ya Kiwalani Fc amelipongeza Jeshi la Polisi mkoa wa Ilala kwa kuleta mashindano haya kwani yanaweka mahusino mazuri kati ya Jeshi la Polisi na raia.
"Hongera kwa Jeshi la Polisi kwani mashindano haya yanaleta mahusiano mazuri kati ya Polisi na raia.
Pia ACP Kunga alikabidhi tuzo kwa Mr. Pritesh ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya *MM steel co ltd* mdau aliyejitokeza kudhamini mashindano ya Polisi Jamii CUP.
Amesema " nikushukuru mdau wetu Mr. Pritesh, uongozi wa shule ya msingi Tabata, serikali za mitaa na wengine wote mliotuunga mkono katika zoezi hili la kimichezo."
Mashindani hayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka baada ya leo kuhitimishwa hivyo timu ambazo hazikufanikiwa kuwa mabingwa zijipange katika awamu nyingime.


Post a Comment