******
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa (takukuru) Ilala Dar es-salaam imesema imegundua uwepo wa mapungufu kwenye utekelezaji miradi mitatu (3) inayoendelea yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.9 jijini hapa.
Akiongea kuhusiana mapungufu hayo wakati akikielezea utekelezaji wa taasisi hiyo kwenye mkoa wa Ilala katika kipindi cha Januari hadi machi 2023 mkuu wa takukuru Ilala sosthenes kibwengo amesema katika kipindi hicho wamebaini mapungufu kwenye miradi mitatu(3),miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.9.
Amesema mradi hiyo ni ujenzi wa maliwato ya umma 30 unatekelezwa na dawasa, ujenzi wa kituo afya segerea na utoaji wa mikopo kwa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu


Post a Comment