IMEBAINIKA kuwa bado wanawake wanaoishi maeneo ya vijijini wanakabiliwa na tatizo la mabadiliko ya Tabia ya nchi inayotokana na kukosa uelewa juu ya masuala ya mazingira.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dodoma ,Fatma Hassan Tawfiq, wakati wa kikao cha masuala mabadiliko ya tabia ya nchi na upatikanaji wa rasilimali fedha kilichoandaliwa na shirika la wated na kuwakutanisha wadau mbalimbali ambao walizungumzia suala la mabadiliko ya tabia ya nchi na uwezeshaji katika suala hilo.
Amesema wanawake wanaoishi maeneo ya vijijini wanakumbana na matatizo ya ukame wanashindwa kuhimili hali hiyo.
"Wanawake kule vijijini tatizo linatokana na uelewa ndio maana wamekuwa waathirika wakubwa wa mabadiliko ya nchi"Amesema Tawfiq
Mbunge huyo amezishauri asasi za kiraia pamoja na serikali kuzidisha nguvu katika kutoa elimu kwa wanawake vijijini ili kupunguza athari za tabia ya nchi kwao.
Naye ,Maria Matui,amesema makundi ya wanawake yapo mbali kufahamu juu mabadiliko ya nchi kutokana na sera zilizopo.
Aidha,Matui amesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,amefanya jitihada kubwa kuongeza Rasilimari fedha katika kutatua changamoto za mabadiliko ya tabia nchini.


Post a Comment