AJALI YA BASI LA NEW FORCE LA YAUA NA KUJERUHI

******

Basi la Newforce lenye namba za usajili T. 173 DZU lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Rukwa limepata ajali katika eneo la kijiji cha Igando mkoani Njombe na kuua watu watano.


Akitoa taarifa za awali Kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe John Imori amesema kuwa mpaka sasa wamethibitisha vifo vya wanaume wanne na mtoto wa kike mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 8 - 9.

Ameongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo la Newforce ambalo lilikuwa likijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake matokeo yake likaacha njia na kugonga daraja na kisha kuangukia mtaroni.

"Kwa sasa tumebaini vifo hivi vya watu watano lakini bado idadi ya majeruhi hatujaipata hivyo tutaendelea kutoa taarifa zaidi kwa kadri tunavyoendelea na zoezi hili".

0/Post a Comment/Comments