*****
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa
cha Mapinduzi (UWT)Mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amewataka wanawake wote nchini kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiliamali lui kujiinua kiuchumi.
Scolastica ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Jumuiya hiyo na kusisitiza kuwa wanawake waweze kuepukana na hali ya utegemezi katika maisha ni vyema kuepukana na tabia ya kukaa bila kujishughulisha huku akiwapongeza wanawake wa mkoa huo kwa kujishughulisha na shughuli ikiwemo ya kilimo hususani cha mazao ya chakula pamoja na biashara likiwemo zao la parachichi.
Amesema ili kutimiza malengo hayo kila mmoja kwa nafasi yake wanapaswa kuhakikisha wanatumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika maeneo yao na kuzitumia wakati wote ili kufikia azma hiyo ambayo viongozi wengi nchini wamekuwa wakilisisitiza.
"Tunapaswa kuamka sasa na kuingia kufanya kazi kwa bidii, hakuna mafanikio yoyote tunayoweza kuyapata kama kama hatutojishughulisha, tutumie fursa zote ambazo tunaziona katika maeneo yetu kujiinua "amesema Mama Kevela
Akitolea mfano katika hilo Kevela amesema chini ya uongozi wake UWT Mkoa huo imeanzisha kiwanda cha WAZAWA NJOMBE PRODUCTS kinachozalisha sabuni ya 'Mama Soap One' kwa lengo la kuhakikisha inajikuza kiuchumi jambo ambalo amesema linapaswa kuigwa na wanachama hao.
Aidha katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa UWT amewataka wanawake hao hususani wa Mkoa huo wa Njombe kuepukana vitendo vya ukatiri wa kijinsia na kuvikemea mahali popote pale vinapojitokeza ndani ya mkoa huo.
Amesema kimsingi vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na mambo mengine vinakwamisha juhudi za maendeleo nchini ikiwa ni pamoja na kuyumbisha misingi ya utamaduni wa mtanzania hivyo jambo jema ni kuhakikisha jamii inaviepuka.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Mkoa wa Njombe Rehema Mbwana amewataka wajumbe wa Baraza hilo hususani Makatibu wa Wilaya na Kata wa Jumuiya hiyo kuhakikisha wanapambana kuongeza idadi ya wanachama ili kuimalisha Jumuiya hiyo.
Amesema kimsingi UWT imejiwekea misingi thabiti kuhakikisha inazidi kujihimarisha sambamba na kukihimarisha chama kwa ujumla hivyo ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anatumia weledi kukijenga chama hicho.
Ends



Post a Comment