Afisa wa TRA mkoa wa mbeya Nicodemus Masawe akizungumza na waandishi wa habari
Meneja wa TRA mkoa wa mbeya Msibu Shabani akizungumza na waandishi wa habari
...........................
Na Richard Mrusha
MENEJA wa TRA Mkoa wa Mbeya, Msini Shabani amesema kuwa kilimo hakitozwi kodi lakini sheria ya mapato ya mwaka 204 sura Namba 332 imeeleza wazi kuwa mtu yoyote mauzo yake yanaanzia Milioni 4 na kuendelea anatakiwa alipe kodi ndiyo maana TRA imetumia fursa ya sherehe za Nane Nane kutoa elimu kwa wakulima pamoja na watanzania kwa ujumla.
Kwa Fursa hiyo meneja huyo wa TRA ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Mbeya kufika katika banda hilo kupata elimu na faida zingine zinazotokana na Maonesho hayo na kusisitiza kuwa licha ya maonesho wananchi wakumbuke kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali na kuonya kuwa wafanyabiashara wasitumia mwanya wa sherehe za Nane Nane kutotoa risiti kwa wateja wao wakifanya hivyo ni kosa kisheria.
Meneja huyo wa TRA Mkoa wa Mbeya aliyasema hayo jana wakati akizungumza na jopo la waandishi wa habari kwenye banda la TRA kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya ambao wamehudhuria maonesho hayo.
Naye Afisa wa TRA kutoka Mkoa wa Mbeya Nicodemus Masawe alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi kwenye banda lake katika maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale ili wapate huduma mbalimbali kutoka TRA lakini wajifunze mambo mengi yanayohusu masuala ya kodi, huku akisema kuwa kwenye TRA kuna misamaha ya kodi na misamaha hiyo imelenga zaidi sekta ya kilimo na kufafanua kuwa wale wote wanaotaka kuagiza matrekta nje ya nchi hayana kodi ili kusaidia kilimo kikuwe kwakuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa letu la Tanzania.
''Matrecta yakiingia kutoka nje yana msamaha wa kodi lakini pia zile nyumba za kupandia mazao (GREEN HOUSE) yakivunywa yaweze kukaa muda murefu, mbolea pia inamsamaha wa kodi na pembejeo nyingine zinazohusiana na kilimo, kwa hiyo wale wote wakulima wadogo, wakati na wakubwa wafike kwenye banda letu ili wajue ni vitu gani vimesamehewa jambo ambalo litawarahisishia katika uwajibikaji wao,'' alisema Nicodemus Masawe afisa kutoka TRA Mkoa wa Mbeya.
Aidha afisa huyo kuhusu sheria ya kodi ya mapato alifafanua kuwa ipo katika makundi mawili namna gani wakulima ama wafanyabiashara wanatakiwa kulipa kodi, kimsingi mkulima anayelima kilimo biashara anatakiwa kulipa mapato, na wanamtambue kwamba sheria inasema mkulima yoyote ikijumuisha mkulima na mfugaji aidha analima mashamba ama anafuga ama mifugo yake kwa mwaka mzima thamani yake ikiwa ni shilingi Milioni 4 huyo hatasajiliwa na TRA kwa kuwa ni kilimo cha kujikimu, lakini kama mkulima mazao yake ama mifugo yake yatazidi milioni 4 huyu ataingia kwenye kodi kwa maana ni mkulima anayelima kibiashara lakini kwenye kutozwa kodi tutaangalia gharama ya kilimo.
Kauri mbiu kwa mwaka huu, ''Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu na chakula''


Post a Comment