FOLENI DAR HUPOTEZA SH 4 BILLIONI KILA SIKU

******
Imeelezwa kuwa  Jiji la Dar-es-Salaam  linapoteza kiasi cha shilingi bilioni 4 kwa siku sawa na tirioni 1 .4 kwa mwaka kutoka na msongamano unaosababishwa na foleni ya magari.

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Ubia Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, David Kafulila katika  kikao cha kukisikiliza mawasilisho zaidi ya manne ya wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali ambayo wanapendelea kuwekeza kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Kafulila amefafanua kuwa upotevu huo unatokana na ukichukua hesabu ya muda wanaotumia kukaa barabarani kwa ajili ya foleni wanapunguza muda wa kazi kwa kiasi gani,mafuta yanayoungua kwa kukaa barabarani kwa muda mrefu ukilinganisha na kama hakuna foleni yani mwendo ambao ungeenda kilomita 50 kwa saa unaenda kilomita 10 kwa saa kwa mfano maana yake hiyo pekee yake inakutafuna mara tano.

Amesema Jiji la Dar-es-Salaam wingi wake wa watu na  maeneo yake halipaswi kuwa na foleni ya kiasi hicho ambapo changamoto pekee ni miundombinu  ndiyo inachangia  kuwa na msongamano.

Hivyo wanatakiwa kukabiliana na changamoto ya miundombinu ambapo zipo njia tatu ikiwemo ya reli ya mjini, barabara za kutoa watu katikati ya jiji pamoja na barabara za mwendo kasi.

0/Post a Comment/Comments