Waziri wa Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) akizungumza wakati
akifungua Jukwaa la Uhuru wa Mtandao Barani Africa 2023(FIFAfrica23) katika
Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 28, 2023.
NA MUSSA KHALID
Serikali imesema licha ya kuwa na Uhuru wa Mtandao barani Afrika ni muhimu kuendelea kulinda tamaduni,watoto na bara la Afrika kwa ujumla ili kuhakikisha jamii inakuwa salama.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameeleza hayo jijini Dra es salaam wakati akifungua Jukwaa la Uhuru wa Mtandao Barani Africa 2023(FIFAfrica23) ambalo limeyakutanisha zaidi ya mataifa 40 Afrika kwa lengo la kujadili faida na changamoto za kimtandao.
Waziri Nape amesema kuwa nchi ya Tanzania ni waumini wa uhuru wa mtandaoni kwani imeweka katika katiba na sheria hivyo amesisitiza kuutumia uhuru huo vizuri ili kuepukana na madhara.
‘Pamoja na Uhuru huo ni muhimu sana kuendelea kuilinda na jamii na Bara la Afrika kwani tuna utamaduni wetu kama bara na watanzania hivyo licha ya kutuunganisha na dunia ni vyema ukatumika vizuri kuhakikisha jamii yetu inakuwa salama kwani tungetamani bara hili liendelee kubaki salama’amesema Waziri Nape
Katika Hatua Nyingine amesema ikiwezekana chaguzi zijazo za kuchagua viongozi mbalimbali nchini ziwe ni zenye kutumia teknolojia kwa mtu kupiga kura popote mtandaoni jambo ambalo pia litaepusha foleni wakati wa zoezi hilo.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Neema Lugangira amesema kuwa kufanyika kwa mkutano nchini inadhihirisha namna Dkt Samia Suluh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amejikita kuimarisha uhuru wa habari,kujieleza na haki za binadamu.
Mbunge huyo pia ameiomba serikali kutoizima mitandao ya kijamii kama baadhi ya nchi za Afrika zimekuwa zikifanya wakati wa uchaguzi ili kuwa uhuru watanzania na wananchi waweze kuona wagombea wao na muendelezo wa kampeni.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa Mkutao huo akiwemo Laibu Leornad ambaye Meneja Masoko Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL amesema ushiriki wao ni kuwawezesha watanzania kupata huduma zote huku Mkurugenzi wa Program ya The Launchpad Tanzania Angella Karashani akisema bado kuna uhitaji mkubwa wa ujumuishi katika mitandao ya kijamii.
Mkutano huo wa siku tatu wa Jukwaa la Uhuru wa Mtandao Barani Africa 2023(FIFAfrica23) umewashirikisha wadau mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Selestine Gervas Kakele, Nancy Kaizilege kutoka UNESCO na wengine wengi wakiwakilisha mataifa yao.


Post a Comment