SERIKALI KUWEKA MAZINGIRARAFIKI YA TEHAMA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Selestine Gervas Kakele akizungumza wakati akifungua Siku ya Wanawake katika Kongamano la 7 la TEHAMA Nchini (TAIC 2023) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 16,2023.

Baadhi ya Washiriki katika Kongamano la 7 la TEHAMA Nchini (TAIC 2023) linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaa, leo Oktoba 16,2023.

......................

NA MUSSA KHALID

Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na teknolojia ya Habari imewahakikishia watanzania kuendelea kuweka mazingira rafiki ya kisera na kisheria katika kuchochea na kuvutia ubunifu katika Tehama ili kuweza kuchochea kasi katika kupambana na umaskini nchini.

Pia imewataka wanawake na wasichana wabuni katika Tehama na kujielekeza katika matumizi ya teknolojia rahisi na rafiki ili Tehama iendeleaa kuongeza mchangowake katika taifa.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia Selestine Kakele wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa  Kongamano la saba la mkutano Mkuu wa Tehama ambalo limewakutanisha wataalamu mbalimbali.

Aidha amesema kuwa sera ya Tehama ambayo wanaipitia kwa sasa ina nguzo sita ikiwa ni pamoja na miundombinu ya uchumi wa kidigitali,usimamizi wa mazingira wezeshi,elimu ya kidigitali na uendelezaji ujuzi,ubunifu,kujenga uchumi wa kidigitali jumuishi na huduma za kifedha za kidigitali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tehama Dkt Nkundwe Mwasaga amesema kuwa kongamano hilo linakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo Tumia teknolojia Ibukizi katika mapinduzi ya kidigitali ili kutengeneza kazi na kuleta mafanikio kiuchumi na kijamii’

‘Katika siku ya kesho tar 17 kwenye kongamano hili tumeweka tehama kwa vijana ikiwa inaendena na mtazamo wa kidunia katika ujumuishi wa kuyashirikisha makundi mbalimbali ambapo tunajadili mafanikio sambamba na kujifunza nchi za nje wao wamefanyaje kuhakikisha uchumi unakwenda vizuri”amesema Dkt Mwasaga

Esta Mengi ni Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Tehama amesema Kongamano hilo ni moja ya hatua kubwa ambayo nchi imeifikia kwa kuweka kipaumbele katika Tehama kwa maendeleo ya jamii.

0/Post a Comment/Comments