VIFO TAKRIBANI 1,545 VIMERIPOTIWA KWA BARA LA AFRIKA PEKEE-CP MARIJAN


................

Takwimu zimeonesha kuwa mwaka 2022 vifo takribani 1,545 vimeripotiwa kwa bara la Afrika pekee vilivyotokana na ajali za usalama barabarani huku watoto wakiwa wahanga wakubwa wa ajali hizo, hayo ni kwa mujibu wa kikosi cha usalama barabarani cha jeshi la polisi Nchini.

Katika kupunguza ombwe la ajali hizo kampuni ya Puma Energy kwa kushirikiana na Amend Tanzania wamezindua kampeni ya kuleta mabadiliko ya usalama barabarani ili kuwawezesha watoto na kuboresha usalama wao iliyopewa jina la ‘’kuwa salama barabarani Afrika.

Akizundua kampeni hiyo Jijini Dar es salaam Kamishna wa jeshi la polisi CP Nsato Marijani amesema kampeni hiyo imeunga mkono moja kwa moja jitihada za serikali katika kutokomeza vifo vinavyotokana na ajali za barabarani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Puma Tanzania Dkt selemani Majige amesema ushirikiano huo utajipambanua katika mikao mingine ili kuweza kuwafikia watanzania wengi zaidi.

Nao baadhi ya wanafunzi walioshiriki uzinduzi huo wamesema kuwa kampeni hiyo itawasaidia kuepukana na ajali huku wakishahuri elimu zaidi iendelee kutolewa.

Shule tano za msingi Jijini Dar es salaam zilizotajwa kuwa na mazingira hataraishi za ajali za barabarani ni pamoja na Shule ya msingi Kibugumo, Kifuru, Msewe, Kibasila na shule ya msingi ya Mtambani.

0/Post a Comment/Comments