DIWANI PASTORY KYOMBIYA AELEZA UTEKELEZAJi WA ILANI KIMANGA

.............................

NA HERI SHAABAN ( ILALA )

Diwani wa Kata ya Kimanga Pastory Kyombiya, aeleza mikakati yake ya utekelezaji wa Ilani kwa kueleza  vipaumbele vyake kwa ajili ya kutatua kero za wananchi. 

Diwani Pastory Kyombiya, alieleza hayo katika tukio la Opresheni Bendera kwa wajumbe wa mashina na mkutano wa Halmashauri kuu wakati wa kukabidhi Bendera kwa wajumbe na Vitendea kazi kwa viongozi wa chama na Jumuiya ambapo wote walipewa kanuni na miongozo matawi yote vifaa hivyo vimetolewa na Diwani huyo .

"Vipaumbele vyangu kata ya Kimanga tutajenga Barabara tano za ndani kwa kiwango cha lami  na Benki ya Dunia baadhi ya Barabara hizo ABC ,Maji chumvi Barakuda,TASAF kwa Makamba,daraja la Kimanga Tabata Bima ,kwa Manyau Nyau kwa Mzava nawaomba wananchi wangu muwe wasikivu Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan  inawajali wananchi na inatatua kero za wananchi "alisema Kyombya.

Diwani Kyombya  alisema wakati mikakati ya utekelezaji wa barabara za kisasa ukiendelea hivi karibuni greda la Halmashauri ya jiji litachonga barabara mbovu zote za Kimanga kwa muda wa wiki moja .

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Chama Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya Elimu Kimanga shule za sekondari na Miradi wa kituo cha afya ,soko la kisasa.

Alisema maendeleo ya Kimanga yataletwa  Wananchi wa Kimanga aliwataka  viongozi wa Kimanga washirikiane katika kufanya kazi zaidi na kutatua kero mbali mbali. 

Katika mkutano huo Diwani Pastory Kyombiya alikabidhi reja kwa wajumbe wa mashina kata nzima ya Kimanga pamoja na Bendera za Wajumbe wa mashina  na miongozo ya chama na kanuni kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa Mwaka 2024 na Uchaguzi  mkuu mwaka 2025 wa Rais Wabunge na madiwani  


0/Post a Comment/Comments