PURA YAGUNDUA VISIMA 44 VYA GESI TANZANIA



                            ********

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema, taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015, imechimba visima vya utafutaji gesi 96.

Amesema, visima 37 vipo baharini na 59 nchi kavu na kwamba, visima 44 viligundulika kuwa na gesi huku. Katika na Kati ya hivyo 16 vipo nchi kavu na 28 baharini.

Mhandisi Sangweni alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wake na wahariri ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina tarehe 6 Novemba 2023.
Amesema, mpaka sasa maeneo yaliyofanyiwa utafiti na taasisi hiyo ni jumla ya Kilometa za Mraba 530,000 ambapo kilometa 394, 000 zipo nchi kavu na 140,000 zipo baharini.

Mhandisi Sangweni amewaeleza wahariri kwamba, kwa sasa Tanzania ina jumla ya mikataba 11 ya utafutaji, uendelezaji na Uzalishai Mafuta na Gesi (PSA) ambapo mitatu ipo katika uzalishaji na minane katika hatua ya ufuatiliaji.

0/Post a Comment/Comments