Wahariri wa habari na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina.
********
Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt, John Mduma amesema, thamani ya mfuko huo hadi kufikia Septemba, mwaka huu ilikuwa shilingi billioni 697.5.
Kwa mujibu wa Mduma, mapato ambayo yanatokana na uwekezaji wa mfuko huo sasa yanafikia zaidi ya Sh300 bilioni.
Dkt Mduma amesema hayo jijini Dar es salaam katika kikao kazi kati ya Jukwaa la Wahariri (TEF), chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).
Amesema kwa sasa mfuko huo unatoa mafao saba ambayo yanajumuisha fao la matibabu, ulemavu wa muda, ulemavu wa kudumu, fao la utegemezi, fao la utengamao na fao la utegemezi.
Amesema fao la utegemezi limelenga kumjengea uwezo mwajiriwa ambaye anapata ajali au ugonjwa kazini uwezo ili aweze kujitegemea licha ya changamoto ambayo amenitia akiwa kazini.




Post a Comment