Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dk JOHN MDUMA alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano wa wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF mkutano ulioandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Tobias Makoba, akizungumza kwenye Mkutano wa wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF mkutano ulioandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina.
*********
Na Mwandishi Wetu.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umelipa kiasi cha shilingi bilioni 65 kwa wanufaika wake.
Malipo hayo ni Hadi kufikia Septemba 30, mwaka huu huku ukiahidi kuendelea kuimarika zaidi kwa maslahi ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa Alhamisi Novemba 2,2023 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dk John Mduma alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano wa wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF mkutano ulioandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina.
Amesema hadi sasa mfuko umetoa malipo ya kodi ya Serikali inayotokana na mapato kiasi cha Sh62.7 bilioni huku akibainisha kuwa hadi kufikia September 2023 mfuko umesajili aslimia 93 ya wanufaika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uendeshaji kutoka WCF, Anselim Peter ameeleza kuwa endepo mfanyakazi akapata ajali eneo la kazi na kupata ulemavu usiozidi asilimia 30 atalipwa fidia kwa mkupuo na kama ikizidi asilimia 30 fidia yake itaingizwa katika mafao ya pensheni kwa maisha yake yote.
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wanufaika wa mfuko huo Hassan Beauty Jackson pamoja na Halima Mbwana kwa pamoja wameeleza namna mfuko huo umekuwa faraja na msaada kwao baada ya kukutwa na changamoto na kutoa rai kwa waajiri kuwasajili watumishi wao katika mfuko huu.
Akizungumza kwa niaba ya wahariri mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF Deodatus Balile amewataka wahariri pamoja na waandishi wa habari kwenda kufikisha taarifa kwa waajiri wao ili wapate haki yao ya msingi ya kujiunga na mfuko huu na kuwasihii mashuhuda waliopata changamoto na kulipwa fidia zao kuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari ili elimu ifikie Umma wa wananchi kwa kiasi kikubwa.
Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi WCF ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi lengo kuu likiwa ni kushughulikia fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta ya Umma na binafsi ambao watumishi wao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazofanya kwa mujibu wa mikataba yao ya ajira.
##MWISHO##




Post a Comment