Na
Sixmund Begashe
Timu
ya wataam kutoka Benki ya Dunia wanaosimamia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa
Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) inayoongozwa na Dkt
Enos Esikuri imefanya zoezi la upandaji miti katika Hifadhi ya Taifa Mikumi
kama sehemu ya mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza
baada ya zoezi la upandaji miti katika Hifadhi hiyo, Dkt. Esikuri amesema,
wameamua kuweka alama ya kudumu kama sehemu ya kuelimisha umma juu ya umuhimu
wa Uhifadhi endelevu wa Ikolojia katika maeneo yaliyohifadhiwa Kisheria.
Dkt.
Esikuri ameongeza kuwa, Hifadhi ya Mikumi inamchango mkubwa kwa uchumi wa
Tanzania hivyo itakapokuwa na uhai wa Ikolojia endelevu itasaidia uhai wa
Wanyamapori ambao ndio kivutio kikubwa cha Watalii wa ndani na nje ya nchi na
kuifanya Tanzania iongeze pato la Taifa litakalo saidia kuinua maisha ya
Watanzania.
Aidha
Dkt. Esikuri na wataalam wengine wa Benki ya Dunia wameendesha zoezi la
upandaji miti Hifadhi ya Taifa Mikumi kama sehemu ya maandalizi ya ya Mapokezi
ya watalii wengi zaidi watakao miminika baada ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege
cha Kikoboga ambao kinajengwa kupitia mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili
na kuboresha Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) unaotekelezwa kwa mkopo wa
masharti nafu kutoka Benki ya Dunia.
Akizungumza
baada ya zoezi la upandaji miti Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi ya
Taifa Tanzania (TANAPA) Kanda ya Mashariki Massana Mwishawa ameipongeza Benki
ya Dunia kwa kuendelea kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika
Uhifadhi endelevu wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania na kuahidi
kuwa TANAPA itahakikisha miti yote iliyopandwa itatunzwa kikamilifu kama urithi
si kwa watanzania tu bali kwa watu wote Duniani hususani kwa watakao tembelea
Hifadhi hiyo.

.jpeg)




Post a Comment