TIMU YA WANAHABARI YATUA MIKUMI KWA REGROW


.................
Na Sixmund Begashe

Timu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali imewasili Mikumi Mkoani Morogoro Kwa lengo la kujionea namna wananchi wanavyonufaika na Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW)

Akizungumza kwa niaba ya Wanahabari hao, Meneja wa Maudhui wa Wasafi Media, Bw Orest Kawau, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa namna inavyo tekeleza Mradi wa REGROW hasa hasa namna unavyo wanufaisha wananchi huku ukiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake.

Bw Kawau ameongeza kuwa, ushirikishwaji wa wanahabari unaofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo, unatoa nafasi ya uelewa mpana kwa waandishi wa Habari juu ya kazi Kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

"Tunaipongeza sana Serikali kwa kazi hii kubwa hapa Mikumi na Sehemu zingine za Mradi huu, tuwahakikishie tu kuwa, ushiriki wetu katika kushuhudia namna Mradi huu unavyo inua maisha ya wananchi unatupa nafasi adhimu ya kuwa mabalozi wa REGROW" aliongeza Bw. Kawau.

Timu hiyo ya Wanahabari ilipowasili Mikumi ilipokelewa na Naibu Msimamizi  wa Mradi Bi. Blanka Tengia, Kaimu Mkuu wa
Hifadhi ya Taifa Mikumi Afisa Mwandamizi wa Uhifadhi Greyson Maro na Maafisa wengine wa REGROW na wa Hifadhi hiyo.

0/Post a Comment/Comments