Mkurugenzi Mtendaji wa
chama cha waagizaji na wasambazaji wa mafuta Tanzania –TAOMAC wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu hali ya biashara ya mafuta hasa
katika kipindi hiki ambacho Tanzania imekumbwa na uhaba wa Dola.
NA ISSA MOHAMMED
Serikali ya Tanzania
imeshauriwa kujipambanua katika matumizi ya nishati asilia ikiwemo Gesi ili
kupunguza utegemezi wa uagizaji mafuta kutoka nje ya Nchi pamoja na
changamoto zingine zinazopelekea upandaji wa mafuta ya petroli na Dizeli.
Ushahuriwa huo umetolewa
Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waagizaji na
wasambazaji wa mafuta Tanzania –TAOMAC wakati akizungumza na mwandishi wa
habari hizi kuhusu hali ya biashara hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho
Tanzania imekumbwa na uhaba wa Dola.
Amesema hatua nyingine
inayopaswa kuchukuliwa na Serikali ni pamoja na kuboresha miundominu ya
kupokelea mafuta katika Bandari ya Dar es salaam ili kupunguza ombwe la kukaa
muda mrefu kwa meli zinazokuja hapa Nchini kushusha mafuta hayo.
‘’Serikali inapaswa
kuwa na njia za muda mrefu wa matumizi ya nishati, kwa mfano matumizi ya –CNG,
hasa katika sekta ya usafiri kwahiyo itasaidia hata uagizaji wa mafuta
itapungua hasa kutumia dola’’ Amesema Mgaya.
Sambamba na hilo Mgaya
amesema chama hicho kimetumia euro milioni 26 katika kipindi hiki cha mwezi
Aprili ili kuagiza mafuta nje ya Nchi kutokana na uhaba wa dola jambo ambalo
limekua likiathiri mwenendo wa biashara hiyo.
‘’Sasa ukioanisha na
dola za kimarekani zilizotumika kuagiza mzigo ambao unauzwa mwezi huu hizo Euro
zilikua asilimia 25, na msambazaji unapaswa kumlipa kwa dola kutokana na
mkataba ndio unatambua dola na sio Euro na hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa
ongezeko la bei.
Aprili 3 Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji –EWURA ilitangaza bei mpya ya mafuta ambapo kwa Jiji la Dar es salaam Petroli imepanda kutoka shilingi 3163 hadi 3257 huku Dizeli ikipanda kutoka shilingi 3126 hadi 3210 huku sababu zilizotajwa na kupanda kwa matumizi ya euro.
Post a Comment