BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) kwa
kushirikiana na kampuni ya Metro Life Assurance wamezindua Bima Benki yenye
lengo la kutoa huduma mbili za Bima ziitwazo ADABIMA na Saccos Schemes Credit
Life.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Mei
17,2024 Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware
amesema kiini cha huduma hizo ni kujenga uelewa wa umuhimu wa elimu katika
kujenga kesho bora ya jamii.
Dkt. Baghayo akizungumzia kuhusu ADABIMA, amesema huduma hiyo ni maalum kwa ajili ya ada
ya shule inayokamilisha kiu ya mzazi au mlezi kumwona mtoto wake akifanikiwa
kwa kupata elimu bora anayostahili ambapo bidhaa hiyo ilithibitishwa na Mamlaka
mnamo tarehe 22 Novemba 2023.
“Kama tujuavyo wote, majanga ni jambo
lisiloepukika katika maisha yetu. Si mara zote mipango yetu inatimia kama
tunavyokusudia. Majanga hutokea katika nyakati tusizotegemea na kuvuruga
mipango yetu na familia zetu.”
“ADABIMA ni suluhisho la changamoto hizi za
maisha, lakini pia ni ahadi kwa wateja kwamba lolote litakalotokea kampuni yake
itasimama pamoja naye kuhakikisha mtoto anasoma na kuhitimu masomo yake bila
kadhia yoyote ile.” Amesema Dkt. Baghayo
Kuhusu Saccoss Schemes Credit Life Insurance,
Dkt. Baghayo amesema ni huduma ya bima maalum kwa ajili ya wadau wa SACCOS na
Vikundi vya huduma ndogo za fedha (micro-finance).
Amesema Mamlaka itahakikisha huduma hiyo inaendelea
kuwapa watumiaji usalama wa kifedha, utulivu, kujiamini na amani.
“Wadau hawa wanajenga kesho iliyo bora kwa
kuinua uwezo wa watoa mikopo na kuwahakikishia wakopaji usalama na umiliki wa
mali zao endapo watashindwa kulipa.” Ameeleza
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Bima
kutoka Benki ya TCB, Francis Kaaya amesema Bima hizo ni kielelezo cha dhamira
ya Benki ya TCB ya kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kadri ya mahitaji yao na
kuwahudumia watanzania kwa ujumla.
“Tunaelewa umuhimu mkubwa wa elimu katika
kujenga kesho bora ya jamii yetu. Bima hii inawapa usalama wa kifedha, lakini
pia inalea ndoto na matarajio ya wateja wetu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Metro Life Assurance, Amani Boma akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life .
.jpeg)



Post a Comment