Kati ya migodi hiyo, migodi mikubwa ni nane, migodi ya kati
56 na migodi midogo 21,622.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Msafiri Mbibo akimwakilisha Waziri wa Madini,
Mhe. Anthony Mavunde katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wakaguzi wa Migodi kutoka
Tume ya Madini uliofanyika leo Mei 30, 2024 katika ukumbi wa Kambarage - Hazina
mjini Dodoma.
Amesema, ukaguzi uliofanyika umewezesha Sekta ya Madini
kuendelea kuimarika na kuongeza makusanyo na mchango wake katika ukuaji wa
uchumi.
“Pamoja na kuimarika
kwa Sekta ya Madini na mchango wake katika ukuaji wa uchumi bado kuna
changamoto za matukio ya ajali katika maeneo ya wachimbaji wadogo ambapo
husababishwa na kuanguka kwa mashimo/maduara ya uchimbaji na ajali zingine
husababishwa kwa kukosekana kwa hewa ndani ya mashimo/maduara,” amesema Mbibo.
Amesema kuwa kutokana
na hali hiyo, Tume ya Madini chini ya Katibu
Mtendaji wake, Mhandisi Yahya Samamba imeagizwa kuimarisha na kuhakikisha ukaguzi unafanyika
mara kwa mara hasa katika maeneo ya wachimbaji wadogo ambapo matukio mengi ya
ajali yamekuwa yakitokea ukilinganisha na maeneo ya wachimbaji wa kati na
wakubwa.
Pia, wametakiwa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wachimbaji
wadogo ambao wengi wana uelewa mdogo wa
masuala ya afya mahala pa kazi na usalama.
“Hivyo mna wajibu mkubwa kuhakikisha mnawasimamia ipasavyo
na kuwaelekeza njia salama za uchimbaji pamoja na matumizi salama ya baruti ili
kuepuka ajali zinazohatarisha usalama wao na kurudisha nyuma jitihada za ukuaji
wa sekta ya wachimbaji wadogo nchini,”amesema na kuongeza,
“ Sisi kama Wizara tunaamini kuwa, uhai wa mchimbaji mmoja
una umuhimu mkubwa kuliko uzalishaji wowote wa madini,”amesema.
Aidha, Mbibo amesema kuwa ili Sekta ya Madini iendelee kukua
na kuchangia asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo Mwaka 2025, wakaguzi wa
migodi wana wajibu wa kuendelea kusimamia na kuimarisha
kaguzi katika maeneo yao ya kazi.
Amesema, sehemu kubwa ya makusanyo yote ya Wizara ya Madini
yanatokana na mrabaha na ada ya ukaguzi, hivyo migodi inaposimama kufanya kazi
kutokana na ajali inaathiri makusanyo
kwa Wizara na Serikali kwa ujumla.
Mbibo pia, amewaagiza wakaguzi wa migodi, kuimarisha kaguzi
katika migodi yote mikubwa, ya kati na hususan migodi ya wachimbaji wadogo
nchini ili kuepusha ajali zinazoweza kutokea na kusababisha kusimamisha
uzalishaji.
“Mkaendelee kutoa elimu juu ya afya, usalama, matumizi
salama ya baruti na utunzaji wa mazingira kwa wachimbaji wote nchini, niwasihi
mkatekeleze majukumu yenu kwa badii kwa kuzingatia uadilifu, uwajibikaji na
waledi, pasipo kujihusisha na vitendo
vya rushwa na pasipo kumuonea mchimbaji yeyote, lakini pia kuendelea
kushirikiana katika kutekeleza majukumu yenu ili kuweza kutimiza lengo,”
amesisitiza Naibu Katibu Mkuu.
Naye, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya
Samamba awali akizungumza amesema sekta ya wakaguzi wa migodi, baruti na
vilipuzi pamoja na ukaguzi wa mazingira ndio injini ya Sekta ya Madini.
Amesema eneo la uchimbaji linapokosa usalama, afya,
mazingira yanapoharibika ndio matokeo ya mwisho
hayawezi kufakiwa.
Mhandisi Samamba amesema kuwa tangu Tume ya Madini ianzishwe
mwaka 2017 na kuanza kazi rasmi Aprili 2018
takwimu za ajali kwa maana ya vifo, ajali na athari za mazingira
zimepungua na kwamba namba hizo hazijapungua
kwa bahati mbaya bali ni kazi kubwa inayofanywa na wakaguzi kwa niaba ya
Tume na kwa kwa maelekezo ya Wizara ya Madini chini ya Mhe. Waziri Anthony
Mavunde (Mb).
“Ukiachia mbali vita ambayo watu wengi wanakufa kwa mara
moja watu 200 hadi 1,000 eneo lingine
linalouwa watu wengi kwa mara moja ni
eneo la uchimbaji, ikitokea madhara watu 40 hadi 50 hupoteza maisha kwa wakati
mmoja.
“Nikuhakikishie kama Tume ya Madini tutaendelea kusimamia
vizuri kupitia kwa wakaguzi wetu wa ndani,” amesema Mhandisi Samamba.
Aidha, amesema kuwa kikao hicho ni maalum kwa ajili ya kujengewa uwezo, kubadilishana uzoefu kwenye shughuli za usimamizi wa migodi nchini.



.jpeg)
Post a Comment