MCHUNGAJI AFARIKI BAADA YA KUPIGWA TEKE NA MUUMINI


 Ibada ya mkesha wa Krismasi katika Wilaya ya Serere Uganda iligeuka kuwa msiba baada ya mchungaji John Michael Ekamu, mwenye umri wa miaka 52, wa Kanisa la Agule Pentecostal Assemblies of God (PAG) kufariki baada ya kupigwa teke na Muumini anayedaiwa kuwa na mapepo

Wakati wa maombi, Osagani alimpiga teke Mchungaji Ekamu, ambaye alianguka lakini aliendelea na ibada hadi asubuhi ya Krismasi.

Asubuhi hiyo, Mchungaji Ekamu alianguka tena madhabahuni. Waumini walipendekeza apelekwe kituo cha afya, lakini alikataa akisema, "shetani ameshindwa."

Hali yake ilipozidi kuwa mbaya, alikubali kupelekwa katika kituo cha afya.-Alifariki wakati wa upasuaji. Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hili.

 cc Bbcswahili

Picha mtandaoni

0/Post a Comment/Comments